1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kibaki ajadili shambulio dhidi ya mkutano wa Uhuru Park Nairobi

Josephat Nyiro Charo14 Juni 2010

Kambi inayopinga katiba mpya imeapa kuendelea na mikutano yao Uhuru Park

https://p.dw.com/p/NqXZ
Waziri mkuu Raila Odinga, kushoto, rais wa Kenya, Mwai Kibaki, katikati, na makamu wake, Kalonzo MusyokaPicha: AP

Rais Mwai Kibaki wa Kenya amekuwa na mkutano wa dharura na maafisa wa ngazi za juu wa usalama nchini humo, baada ya mripuko wa bomu kuwaua watu watano katika mkutano wa kisiasa. Kikao hicho cha faragha kimehudhuriwa pia na makamu wa rais Kalonzo Musyoka na waziri wa ulinzi, profesa George Saitoti.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu wa Nairobi, Alfred Kiti, shambulio hilo ambalo pia liliwajeruhi watu 80, lilitokea katika mkutano wa hadhara mjini Nairobi, ulioitishwa na wale na upande unaopinga rasimu ya katiba mpya itakayopigiwa kura ya maoni Agosti 4.

Wakati huo huo, upande unaopinga rasimu ya katiba mpya umeapa kuendelea na kampeni zao, hata baada ya mkutano wao hapo jana kushambuliwa na guruneti jijini Nairobi.

Aboubakar Liongo amezungumza na mwenyekiti wa chama cha kutetea haki na maendeleo nchini humo, Okia Wamutata, ambaye ni miongoni mwa wale walioko katika kundi hilo.