1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kibaki awaaga wana Afrika Mashariki

Admin.WagnerD21 Februari 2013

Rais Mwai Kibaki wa Kenya amehimitimisha ziara ya siku mbili nchini Tanzania kwa kuwaaga wananchi wa taifa hilo huku akihimiza kuzidisha ushirikiano wa ujirani mwema baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

https://p.dw.com/p/17ixH
Kibaki.jpg ***Kibaki nach heftigen Protesten in Kenia gesprächsbereit *** ** FILE ** Kenya's President Mwai Kibaki is seen in Nairobi in this Dec. 12, 2007 file photo. Kibaki was re-elected in the closest presidential election in the country's history, the elections chief said Sunday, Dec. 30, 2007. The contest was marked by allegations of rigging on both sides. (AP Photo/Sayyid Azim, File)
Rais Mwai Kibaki wa KenyaPicha: AP Photo

Kabla ya kuhitimisha ziara hiyo, Rais huyo wa Kenya alikuwa na mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete baada ya leo mchana kufungua bara bara iliyopewa jina lake.

Rais Kibaki ambaye aliambatana na ujumbe wa maafisa kadhaa, ametumia ziara hio kutoa shukurani kwa wananchi wa Tanzania ambao amewalezea kama marafiki wema kwa Kenya na amehaidi kuendelea kushirikiana nao hata atapoondoka madarakani baada ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika March 4.

Kwa heri Afrika Mashariki

Rais Kibaki ametumia jukwaa la Tanzania kutoa salamu za kwa heri kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kile kinachoelezwa kuwa kama moja ya agenda yake ya kutambua diplomasia yaTanzania ambayo ilifanikisha kumaliza mzozo uliozuka baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007.

Tamko kuhusu uchaguzi wa Kenya

Katika kikao na mwenyeji wake, Rais Kikwete, viongozi wote wawili wamezungumzia uchaguzi mkuu ujao wa Kenya na wakayataka madola ya magharibi kutoingilia kati kwa namna yoyote ile. Rais Kikwete hata hivyo ametaka kufanyika kwa uchaguzi wa haki na huru ili kuepuka hali yoyote ya sintofahamu.

Tanzania's President Jakaya Kikwete speaks during a press availability with Secretary of State Hillary Rodham Clinton at the State House in Dar es Salaam, Tanzania, Monday, June 13, 2011. (Foto:Susan Walsh, POOL/AP/dapd)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa TanzaniaPicha: dapd

Kwa upande wake rais Kibaki amasema kuwa yuko tayari kukabidhi madaraka kwa mgombea yoyote atayeshinda katika uchaguzi huo ambao unatupia macho na Jumuiya za kimataifa. Kuhusu uimarishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Mwai Kibaki alizitaka nchi wanachama kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa madai kuwa ndiyo lugha mama inayoweza kuwaunganisha wananchi wa eneo hili.

Sikiliza ripoti ya George Njogopa kutoka Dar es Salaam, kwa kubonyeza alama ya kusikiliza masikioni hapo chini.

Mwandishi:George Njogopa
Mhariri:Yusuf Saumu