1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Majaji watishwa katika juhudi za kuumaliza mzozo wa kisiasa

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAt

Majaji watano wa mahakama ya katiba nchini Ukraine wamesema mbinyo wa kisiasa na vitisho vinazuia juhudi zao za kuumaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Mahakama ya katiba imeulizwa kuamua ikiwa rais Viktor Yuschenko anayeegemea mataifa ya magharibi na ambaye kwa miezi kadhaa amekuwa haelewani na bunge na waziri mkuu Viktor Yanukovich, alivunja sheria kwa kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema.

Mahakama hiyo ilitarajiwa kupitisha uamuzi wake hii leo lakini imeahirisha kazi hiyo hadi Jumanne wiki ijayo.

Rais Yuschenko ameupongeza msimamo wa majaji hao wa mahakama ya katiba akipendekeza atakuwa tayari kubadili tarehe ya uchaguzi mpya unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 mwezi ujao.

Waziri mkuu Viktor Yanukovich amesema hatashiriki katika uchaguzi ambao bado unasubiri uamuzi wa mahakama.