1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Rais wa Ukraine ashikilia kuvunja bunge

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBZ

Rais Viktor Yuschenko wa Ukraine amesema ataendelea na mpango wake wa kulivunja bunge, licha ya kufanywa maandamano ya kupinga uamuzi huo.Katika hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni,Yuschenko alisema,uamuzi wake ni halali na unafuata katiba.Akaongezea kueleza kuwa alilazimika kutoa amri ya kulivunja bunge na kuitisha chaguzi mpya mwezi wa Mei,baada ya idadi kadhaa ya manaibu wake wanaoelemea upande wa magharibi,kubadilisha utiifu wao na kujiunga na waziri mkuu Viktor Yanukovich anaeiunga mkono Urussi.Yanukovich ameliambia bunge lipinge amri ya Yuschenko.Waandamanaji wa pande zote mbili, kwa maelfu wamekusanyika katika mji mkuu Kiev.