1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Waziri Steinmeier akutana na viongozi wa Ukraine

6 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUZ

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier hii leo anakutana na viongozi wa Ukraine mjini Kiev.Akiiwakilisha Ujerumani ambayo hivi sasa imeshika wadhifa wa urais wa Umoja wa Ulaya,Steinmeier anakutana na waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Volodymyr Ohryzko na rais Viktor Yuschenko kujadili kinaganaga makubaliano mapya ya ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Ukraine. Makubaliano hayo yaliidhinishwa mwezi wa Januari na mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya. Siku ya Jumatatu,waziri Steinmeier alikutana na waziri mwenzake wa Urussi,Sergei Lavrov mjini Moscow.Majadiliano yao yalihusika na masuala ya nishati,biashara na ushirikiano pamoja na Umoja wa Ulaya.Siku ya Jumatano,Steinmeier anaelekea Serbia,ambako atalijadili suala linalohusika na mustakabali wa Kosovo.