1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Yuschenko huenda akakiuka amri yake

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAj

Maandamano ya pande mbili wapinzani yamefanyika katika mji wa Kiev nchini Ukraine.

Msaidizi mkuu wa rais Viktor Yuschenko amedokeza kuwa huenda rais huyo akakiuka agizo lake la kutaka bunge livunjwe na pia kufanyika uchaguzi wa mapema ili kutatua mzozo wa kisiasa unaoikabili Ukraine.

Waziri mkuu Viktor Yanukovych anaelaumiwa kutaka kunyakuwa madaraka amepinga agizo hilo la rais Yuschenko, amesema kwamba amri hiyo ya rais Yuschenko ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Mahakama ya katiba nchini humo imeakhirisha kusikiliza malalamiko hayo hadi wiki ijayo.