1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV:Uchaguzi wa bunge kumaliza mivutano ya kisiasa

30 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLP

Wananchi wa Ukraine wamepiga kura ya kulichagua bunge jipya katika uchaguzi uliowekewa matumaini ya kuumaliza mzozo wa kisiasa.Rais Viktor Yushenko na waziri mkuu Viktor Yanukovich wote wanataraji kwamba uchaguzi huu utakuwa suluhisho la mivutano ya kisiasa kati ya kambi inayoegemea upande wa nchi za magharibi na ule unaoungwa mkono na Urussi.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema asubuhi na matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kuanza kutangazwa wakati wowote kutoka sasa huku matokeo rasmi yakitarajiwa kutangazwa kuanzia kesho asubuhi.

Hata hivyo hakutarajiwi kupatikana mshindi wa moja kwa moja na huenda kukawa na mazungumzo ya kutafuta serikali ya mseto.