1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV:Wabunge kuidhinisha uchaguzi

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvs

Wabunge nchini Ukraine wanaanza kupigia kura miswada itakayowezesha uchaguzi wa mapema kufanyika baada ya Rais Viktor Yuschenko kuongeza muda wake wa mwisho.Hatua hiyo inaipa bunge siku moja zaidi kujaribu kutafuta suluhu ya mkwamo wa kisiasa uliodumu kwa miezi miwili.

Nchi ya Ukraine imekumbwa na mkwamo wa kisiasa tangu Rais Yuschenko kuvunja bunge Aprili 2 na kuitisha uchaguzi wa mapema.Kulingana na Waziri mkuu Viktor Yanukovich na muungano tawala unaomuunga mkono agizo hilo lilikiuka sheria na kukata rufaa katika Mahakama ya katiba.

Viongozi hao wawili walikubaliana siku ya jumapili kuruhusu bunge kupiga kura mwisho wa mwezi Septemba kwa kuhofia kuzuka kwa ghasia nchini humo.Rais Yuschenko hii leo amelipa bunge siku moja ya ziada kuidhinisha miswada hiyo ili uchaguzi ufanyike.