1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI : Wafungwa 8,000 wa mauaji ya kimbari waachiliwa

20 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQX

Serikali ya Rwanda imewaachilia huru zaidi ya wafungwa 8,000 wanaotuhumiwa kwa makosa ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini humo.

Serikali imesema hatua hiyo imekusudia kupunguza msongamano wa wafungwa kwenye magereza ya Rwanda na kwamba kati ya hao walioachiliwa hakuna alie mhusika mkuu wa mauaji hayo.

Zaidi ya wafungwa 60,000 wameachiliwa tokea mwaka 2003 wakati Rais Paul Kagame wa Rwanda alipotangaza msamaha kwa watuhumiwa.

Watutsi na Wahutu walio na msimamo wa wastani zaidi ya 800,000 waliuwawa katika mauaji hayo ya kimbari yaliotokea nchini Rwanda miaka 13 iliopita.