1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI:Ufaransa kushawishiwa kumrejesha Mnyarwanda wanayemzuia

19 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7ET

Nchi ya Rwanda inatoa wito kwa Ufaransa kumrejesha nyumbani raia mmoja wa Rwanda anayesakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kwa ajili ya Rwanada ICTR kwa madai ya kuhusika na mauaji ya halaiki ya mwaka 94.

Rwanda inatoa wito kwa Ufaransa kumrejesha Dominique Ntawukuriryayo aliyekuwa kiongozi wa eneo la kusini mwa Gisagara wakati wa mauaji hayo.Mshukiwa huyo anazuiliwa na polisi wa Ufaransa baada ya kukamatwa kuisni mwa Ufarabsa katika eneo la Carcassonne.