1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI:Wafungwa 20 wanaotuhumiwa katika mauaji ya halaiki wauawa

24 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfk

Polisi nchini Rwanda wamewaua takriban wafungwa 20 tangu mwezi Novemba mwaka jana kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch inayotoa wito wa kufanywa uchunguzi.

Kwa mujibu wa shirika hilo wengi wa wafungwa hao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya mwaka 94 nchini humo na wansubiri kuhukumiwa.Baadhi yao wanalaumiwa kuhusika na visa vya ubakaji na wizi.

Ripoti hiyo inatolewa baada ya kuhoji familia za wahusika na mashahidi.Serikali ya Rwanda bado haijatoa tamko lolote mpaka sasa.Nchi ya Rwanda inaendelea na juhudi za kujenga upya nchi baada ya mauaji ya halaiki ya mwaka 94 yaliyosababisha vifo vya takriban watu laki 8.

Mauaji hayo yalianza baada ya ndege ya Rais Juvenal Habyarimana kudenguliwa ilipoelekea katika mji mkuu wa Kigali.