1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kijana akamatwa Pakistan kuhusu mauaji ya Bhutto

19 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cugl

ISLAMABAD: Maafisa wa usalama nchini Pakistan wanasema, wamemkamata kijana,ikidaiwa kuwa amehusika na mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Benazir Bhutto yaliyotokea mwezi wa Desemba. Mshukiwa huyo mwenye miaka 15 amewaambia wachunguzi kuwa yeye ni miongoni mwa kundi la watu 5 lililopelekwa mjini Rawalpindi,siku ambayo Bhutto aliuawa.

Lakini msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani mjini Islamabad amesema,hana habari zo zote juu ya kukamatwa kwa kijana huyo wala matokeo mapya kuhusu kesi ya Bhutto.