1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kilele cha maandamano ya wakulima Berlin

Sudi Mnette
15 Januari 2024

Idadi kubwa ya matrekta yanaingia katika viunga vya mjii mkuu wa Ujerumani, Berlin kwa maandamano mengine makubwa ya wakulima kupigania hali njema.

https://p.dw.com/p/4bFLk
Berlin | Großdemonstration Bauernproteste
Picha: Florian Gaertner/photothek/IMAGO

Matrekta hayo yatapiga honi katika maeneo kadhaa ya vitongoji vya vya jiji la Berlin kama sehemu ya kuonesha kuchoshwa na hatua ndogo za serikali katika kuyalinda maslahi yao. Wadau wengine katika sekta ya kilimo vilevile wameonekana kuunga mkono maandamano hayo.

Lakini baadae mchana idadi hiyo kubwa ya wakulima kutoka katika maeneo yote ya Ujerumani inatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika eneo maarufu la Lango la Brandenburg kwa kupinga kodi katika mafuta ya dizeli.

Maandamano ya kilele kwa juma zima kwa sekta ya kilimo

Berlin | Großdemonstration Bauernproteste
Maandamano ya wakulima katika viunga vya jiji la BerlinPicha: Florian Gaertner/photothek/picture alliance

Haya ni maandamano ya kilele ambayo yamedumu kwa takribani juma zima. Mapema Asubuhi idadi kubwa ya matrekta iliyonekana katika maegesho ya barabara. Katika mkutano huo wa mchana, wawaikilishi wa vyama vya wakulima, vyama vya wafanyakazi pamoja na Waziri wa Fedha wa Ujerumani Christian Lindner wapata nafasi ya kuzungumza.

Wakulima katika kipindi hiki wametoa malalamiko yao kwa serikali, Luisa Hochstein ni mfugaji:

"Kama mambo yataendelea kwa namna hii, mashamba madogo ya familia kama haya tuliyonayo hapa hayatoendelea. Na labda kilimo cha Ujerumani hakitakuwapo tena, endapo tusipokuwepo basi bidhaa zitaagizwa kutoka nje. nje ya nchi lakini pia hatotofahamu zinazalishwa chini ya hali gani"

Matrekta takriban 5,000 kuzunguka katika viunga vya Berlin

Kutwa nzima ya jana Jumapili, wakulima kutoka kila pembe ya Ujerumani walikuwa wanaelekea mjini Berlin ambako inaaminika takribani matreta 5,000 na malori 2,000 yatanatarajiwa kushiriki katika maandamano hayo. Kwa ujumla idadi ya watu 10,000 inakadiriwa kuwa itajitokeza katika maandamano hayo.

Jana Jumapili, kulikuwa na taarifa za polisi kusimamisha matrekta kuingia katika eneo la ofisi za serikali mjini Berlin. Maandamano hayo yaliyoanza Jumatatu iliyopita yameongeza shinikizo kwa serikali ya mseto ya Kansela Olaf Sholz ambayo bado inahangaika kutatua mzozo kuhusu bajeti ya mwaka ujao.

Soma zaidi:London, Berlin waandamana kupinga chuki kwa Wayahudi, kwengineko kuipinga Israel

Shinikizo la wakulima limeilazimisha serikali kufutilia mbali mipango ya kuondoa nafuu ya kodi kwenye vyombo vya moto vinavyotumika kwa kilimo pamoja na kupendekeza kuondoa kwa awamu ruzuku inayotolewa na serikali kwenye mafuta ya Dizeli yanayoendesha mitambo mashambani.

Vyanzo: DPA