1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga chaua watu wanane.

26 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTHW

Manila. Kiasi watu wanane wameuwawa kutokana na kimbunga Mitag, ambacho kimesababisha mafuriko makubwa na maporomoko ya matope katika milima kaskazini mwa Philippines. Majimbo sita hayakuwa na umeme kwa muda kwa mujibu wa maafisa wa maeneo hayo. Kimbunga hicho ambacho kinapungua kasi hivi sasa kinaelekea Taiwan kikiwa na upepo unaokwenda kasi ya kilometa 150 kwa saa. Wakati huo huo idara ya utabiri wa hali ya hewa imeonya kuwa kimbunga Hagibis , ambacho kimeuwa watu 13 wiki iliyopita, kinatarajiwa kurejea tena nchini Philippines kikiwa na kasi ndogo katika muda wa saa 48 zijazo.