1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Irene chapungua kasi

Abdu Said Mtullya29 Agosti 2011

Jiji la New York laepuka madhara ya Kimbunga"Irene"

https://p.dw.com/p/12PAA

Kimbunga Irene hakikusababisha madhara makubwa katika jiji la New York kama ilivyohofiwa hapo awali.

Meya wa jiji hilo Michael Bloomberg amesema hakuna watu waliokufa wala waliojeruhiwa kutokana na kimbunga hicho. Na kwa mujibu wa taarifa za waandishi wa habari dhoruba hiyo haikuleta madhara makubwa.

Wakati huo huo, idara ya usafiri wa anga imesema kuwa viwanja vya ndege vitatu muhimu,vilivyofungwa hapo awali kutokana na kimbunga Irene, vinatarajiwa kufunguliwa tena leo asubuhi.Lakini huduma kamili zinatarajiwa kurejeshwa hapo kesho .

Kimbunga Irene kilisababisha vifo vya watu wasiopungua 18 jumamosi iliyopita na kuleta hasara ya mabilioni katika sehemu zingine za Marekani.

Akizungumzia juu ya kimbunga hicho Rais Obama alisema mjini Washington kuwa hatari bado ingalipo kutokana na uwezekano wa kutokea mafuriko na kukatika huduma ya umeme .