1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinara wa Umoja wa Mataifa yuko Rwanda

29 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CzLx

KIGALI:

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa-Ban Ki-moon ameanza leo ziara yake ya siku moja nchini Rwanda,huku kukiwa na wingu la kinyongo kwa baraza hilo kushindwa kuzuia mauaji ya halaiki yaliyotokea nchini humo mwaka wa 1994.

Bw Ban Ki-moon aliewasili huko jana,alikwenda kwenye makumbusho ya mauaaji ya halaiki mjini Kigali ili kutoa heshima zake kwa wahanga wa mauaji hayo, yaliyosababisha watu laki nane kuawa,wengi wakiwa wa kabila la WaTutsi.

Aidha amepangiwa kukutana na rais Paul Kagame kwa mazungumzo pamoja na viongozi kadhaa wa serikai kabla ya kuelekea Addis Ababa Ethiopia kuhudhuria mkutano wakilele wa Umoja wa Afrika wa viongozi wa nchi za kiafrika.