1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINGSTON: Kimbunga Dean kinazidi nguvu Bahari ya Karibean

19 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXe

Kimbunga DEAN kinachovuma katika Bahari ya Karibean,kimeua watu wasiopungua 5 nchini Haiti na Jamhuri ya Dominika.Kimbunga hicho sasa kinaelekea pwani ya Jamaika kwa mwendo wa zaidi ya kilomita 200 kwa saa.Wakazi wengi wamekimbilia sehemu za ndani na watalii wanahangaika kupata ndege za kuwarejesha makwao.

Kimbunga hicho pia kinatazamiwa kufika Mexiko Jumatatu jioni au Jumanne asubuhi.Makampuni ya usafiri ya Ulaya,yamefuta misafara ya ndege katika eneo la Karibean kwa muda wa siku chache zijazo.Nchini Kuba pia hatua za tahadhari zimeanza kuchukuliwa kwa usalama wa raia na watalii.