1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINGSTON: Uchaguzi mkuu wafanyika leo Jamaica

3 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBT6

Wajamaica wamejitokeza kwa wingi hii leo kushiriki katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo. Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kukaribiana huku chama kikuu cha upinzani cha Jamaican´s Labour Party kikiendelea kujiimarisha dhidi ya chama tawala cha People´s National Party.

Uchaguzi huo umegubikwa na machafuko baada ya watu waliokuwa wamejihami na bunduki kuwapiga risasi na kuwaua watu saba juzi Jumamosi katika tukio linaloshukiwa kuwa shambulio lililochochewa kisiasa.

Takriban raia milioni 1.3 kati ya raia milioni 2.8 wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi huo.

Upigaji kura ulicheleweshwa kwa wiki moja kufuatia kimbunga Dean kilichosababisha uharibifu mkubwa nchini Jamaica siku 15 zilizopita. Hali mbaya ya hewa inatarajiwa hii leo huku kimbunga Felix kikipita karibu na kisiwa hicho, kilomita kadhaa kusini mashariki mwa nchi hiyo.