1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Hali ni ya kutisha kiasi jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakati ukikaribia uchaguzi wa urais

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1P

Kikosi cha majeshi ya Umoja wa mataifa cha kulinda amani katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo MONUC, kinachunguza harakati za kijeshi kwenye vituo vya kijeshi mjini Kinshasa wakati ikikaribia duru ya pili ya uchaguzi wa urais tarehe 29 mwezi huu.

Hali hiyo isiokuwa ya kawaida katika kambi za kijeshi imefuatia ripoti za matukio mbali mbali katika maeneo kadhaa kati ya wafuasi wa wagombea wawili wa kiti cha urais wanaosalia, rais Joseph Kabila na mpinzani wake Jean- Pierre Bemba.

Hali imezidi kuwa ya kutisha wakati zikisalia siku chache ili ufanyike uchaguzi huo. Duru ya kwanza ya uchaguzi iliofanyika mwezi Julai mwaka huu, ilikwenda salama kwa jumla licha ya matukio mbali mbali.