1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Je kuna ushahidi wa kutosha dhidi ya Lubanga!

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuX

Mahakama ya Kimataifa kuhusika na Uhalifu ICC-imekutana kuamua ikiwa kuna ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi dhidi ya mwanamgambo wa Kikongo anaetuhumiwa kuchukua watoto kupigana vita. Kiongozi wa kundi la wanamgambo nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,Thomas Lubanga mwenye umri wa miaka 45 anatuhumiwa kuwa alitumia watoto elfu kadhaa kama wanajeshi.Mahakama hiyo ya Kimataifa iliundwa mwaka 2002 kama mahakama ya kwanza ya kudumu kusikiliza kesi za uhalifu za mtu mmoja mmoja.