1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Kabila ametoa mwito wa kubakia shwari

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsQ

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ametoa mwito wa kubakia shwari,baada ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi wa rais kwa kujinyakulia zaidi ya asilimia 58 ya kura. Alipozungumza muda mfupi baada ya Halmashauri Huru ya Uchaguzi kuthibitisha ushindi wake,Kabila alitoa mwito kwa wananchi wenzake kuonyesha „udugu na ustahmilivu“ kufuatia kampeni kali ya uchaguzi na mapambano kati ya makundi hasimu,yaliyosababisha hasara ya maisha.Mpinzani wa Kabila,makamu wa rais Jean-Pierre Bemba, amejipatia asilimia 42 ya kura zilizopigwa. Kufuatia madai ya wafuasi wa Bemba kuwa kumefanywa udanganyifu katika kuhesabiwa kura,Halmashauri Huru ya Uchaguzi imehakikisha kuwa uchunguzi utafanywa kuhusu tuhuma hizo. Kabla ya Kabila kuweza kuapishwa tarehe 10 Desemba,matokeo hayo ya uchaguzi lazima yathibitishwe na Mahakama Kuu ya Kongo.