1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Kabila amteua Gizenga kuwa waziri mkuu

31 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCeY

Rais Joseph Kabila wa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo amemtangaza, Antoine Gizenga kuwa waziri mkuu wa serikali yake. Gizenga alitarajiwa kuteuliwa katika wadhifa huo kufuatia hatua yake ya kumuunga mkono rais Kabila wakati wa uchaguzi wa rais uliofanyika hivi majuzi nchini humo.

Gizenga alikuwa zamani makamu wa kiongozi wa kwanza wa Kongo, Patrice Lumumba, aliyeuwawa muda mfupi baada ya Kongo kupata uhuru kutoka kwa Ubelgiji mnamo mwaka wa 1960.