1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Korti kuu yachomwa moto jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

22 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqU

Wafuasi wa kiongozi wa zamani wa waasi katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Jean Pierre Bemba, wameichoma moto hapo jana korti kuu wakiyapinga matokea ya uchaguzi wa urais wa hivi karibuni. Magari ya kijeshi ya kikosi cha Umoja wa mataifa cha kulinda amani nchini Congo yaliingilia kati na kufiatua risase za kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wameanza kuyachoma moto hata magari ya polisi.

Uharibifu huo ambao ulitokea nyakati za adhuhuri, ulisitisha kikao cha korti kuu, kusikiliza kesi juu ya mashtaka ya wizi wa kura yaliowasilishwa na muungano wa vyama vinavyomuunga mkono Jean Pierre Bemba. Kulingana na matokeo ya uchaguzi, Bemba alipoteza katika ushindani na rais Joseph Kabila.