1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Madini ya sumu yatupwa katika mto.

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79F

Maafisa nchini jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo wamenzisha uchunguzi juu ya kutupwa kwa tani 18 za madini yenye sumu katika mto kusini mashariki ya jimbo la Katanga. Madini hayo ni pamoja na tani 17 za shaba ya chenga chenga ikiwa na kiwango kikubwa cha sumu kiasi cha mara 50 kuliko kiwango kinachoweza kuvumilika, zilizokamatwa mwezi uliopita kusini mwa mji wa machimbo ya migodi wa Likasi katika jimbo la Katanga zikiwa zinapelekwa nje ya nchi kuuzwa.

Maafisa waliamuru madini hayo kumwagwa katika machimbo yaliyoachwa ya madini ya Uranium wiki iliyopita , lakini wafanyakazi waliyamwaga karibu na daraja karibu kilometa 10 kutoka Likasi mji ambao una wakaazi wapatao laki tatu.