1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Maeneo ya Mweka na Luebo yawekwa karantini

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQP

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,maeneo yanayozingira Mweka na Luebo yamewekwa karantini ili kuzuia kuambukiza homa ya Ebola ambayo haina tiba.Maafisa wa afya wamesema,homa ya Ebola katika kipindi cha miezi minne iliyopita,imeua zaidi ya watu 160 miongoni mwa wagonjwa 352 kwenye wilaya ya Kasai Occidental.Shirika la Afya Duniani-WHO mjini Geneva limesema,haijulikani kama vifo hivyo vyote vimesababishwa na Ebola kwani kuna magonjwa mengine pia katika eneo hilo.

Waziri wa Afya wa Kongo,Viktor Makuenge Kaput amesema,sampuli tano zilipelekwa katika maabara nchini Gabon na “Kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa,“kimethibitisha kuwepo kwa virusi vya Ebola.