1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Majeshi yaudhibitzi tena mji mkuu

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCG6

Majeshi ya serikali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yamesema kwamba wameudhibiti tena mji mkuu wa Kinshasa kufuatia mapigano ya siku mbili na wapiganaji wa kiongozi wa zamani wa waasi Jean- Piere Bemba.

Maafisa wa serikali wa hospitali wanasema takriban watu 60 wameuwawa na wengine madarzeni kujeruhiwa.Mapigano hayo yalianza hapo Alhamisi wakati wanamgambo wa kikosi cha binafsi cha Bemba walipokaidi agizo la serikali la kuwataka wasalimishe silaha zao.

Mapigano hayo ni ya kwanza kuzuka katika mji mkuu wa Kinshasa tokea Bemba aliposhindwa na Joseph Kabila katika marudio ya uchaguzi wa rais hapo mwezi wa Oktoba mwaka jana.

Bemba ameomba hifadhi katika ubalozi wa Afrika Kusini licha ya mwanasheria mkuu kutowa hati ya kukamatwa kwake kwa madai ya uhaini.