1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Mapigano yatokea kabla ya uchaguzi hapo Jumapili.

27 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyr

Kiasi watu wanne wameuwawa jana katika mapigano baina ya kambi mbili hasimu za kisiasa na watu wengine wanne wamekufa katika ghasia zilizotokea sehemu nyingine, katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, na kuzidisha hali ya wasi wasi wakati nchi hiyo inaelekea katika uchaguzi wa rais mwishoni mwa juma.

Mapigano hayo yalitokea katika mji wa Gbadolite, kaskazini mwa nchi hiyo, ambako waungaji mkono wa mgombea urais Jean-Pierre Bemba walishambuliana na walinzi wa Nzanga Mobutu , ambaye anamuunga mkono rais Joseph Kabila.

Miongoni mwa wale waliouwawa ni pamoja na mmoja kati ya wanajeshi wa jeshi la Bemba , kwa mujibu wa makao makuu ya jeshi la umoja wa mataifa katika mji wa Mbandaka, mji mkuu wa jimbo la magharibi la Equateur ambako mji wa Gbadolite upo.

Jeshi la Monuc limesema kuwa polisi watatu pia wameuwawa na mmoja kati ya walinzi wa Mobutu amejeruhiwa.