1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Serikali mpya yatangazwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

6 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUa

Baada ya kuchelewa kwa majuma kadhaa,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imeichagua serikali mpya.Waziri Mkuu Antoine Gizenga aliteuliwa na rais Joseph Kabila tangu mwezi wa Desemba na mawaziri wengine ndio walitangazwa siku ya Jumatatu kupitia televisheni ya taifa.Waziri mkuu Gizenga mwenye umri wa miaka 81 na mawaziri wake, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuijenga upya nchi iliyoteketezwa kwa vita vya muda mrefu.Nchi sita za jirani zilijiingiza pia katika vita hivyo na kusababisha maafa makubwa ya kiutu. Inakadiriwa kuwa hadi watu milioni 4 wameuawa katika vita hivyo kati ya mwaka 1998 na 2003.