1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Wakongomani kumchagua rais mpya.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCy6

Upigaji kura unaendelea katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo katika uchaguzi wa duru ya pili wa rais.

Uchaguzi huo ni kati ya wagombea wawili, rais wa sasa Joseph Kabila dhidi ya kiongozi wa zamani wa waasi Jean – Pierre Bemba .

Wagombea wote wawili wameahidi kutekeleza sheria za uchaguzi na kuwataka waungaji mkono wao kuwa watulivu baada ya kiasi cha watu 23 kuuwawa katika mapigano ambayo yamefuatia uchaguzi wa duru ya kwanza hapo Julai 30.

Uchaguzi huo wa duru ya pili unakamilisha uchaguzi wa kwanza wa taifa hilo wa kidemokrasia katika muda wa miaka 40.

Upigaji kura unaangaliwa na wachunguzi zaidi ya 1000 wa kimataifa , pamoja na jeshi la umoja wa Ulaya la kulinda amani chini ya uongozi wa Ujerumani.

Matokeo hayatarajiwi hivi karibuni.