1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Wanajeshi 149 wa Bemba wasalimisha silaha

6 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCE

Jumla ya wanajeshi 149 wafuasi wa kiongozi wa zamani wa waasi wamesalimisha silaha zao baada ya kujisalimisha katika kambi ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokarasi ya Congo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Michele Montas amesema wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Congo wanajadiliana na serikali kuhusiana na kuwakabidhi wanajeshi hao kwa mamlaka ya serikali ili kujumuishwa kwenye jeshi la taifa.

Wanajeshi hao ambao walikuwa wafuasi wa mbabe wa vita wa zamani Jean- Piere Bemba walianza kujisalimisha mwezi uliopita baada ya mapigano ya siku mbili kati ya wanamgambo wa Bemba na vikosi vya usalama kuuwa watu 150.

Kufuatia mapigano hayo Bemba alikimbilia ubalozi wa Afrika Kusini kujihifadhi na walinzi wake wakatimka.