1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Watu wenye silaha wakimbia na mafaili.

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwD

Kundi la watu wenye silaha walikodishwa na mmoja kati ya wagombea wa kiti katika uchaguzi wa mabaraza ya majimbo , ambaye hakuridhishwa na hali ya mambo jana lilishambulia ofisi ya tume ya uchaguzi katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na kuondoka na nyaraka kadha.

Tume huru ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa, mgombea katika uchaguzi wa baraza la majimbo , akitambua kuwa matokeo ya uchaguzi yanakwenda kinyume na matarajio yake , aliwakusanya watu wanaomuunga mkono ambao walikwenda katika ofisi ya tume ya uchaguzi katika mji wa Dekese katika jimbo la Kasai Orient.

Msemaji wa tume hiyo Dieudonne Miromo amesema kuwa baadhi ya watu hao walifika katika ofisi hiyo wakiwa na mapanga, pinde na mishale.

Walichukua baadhi ya mafaili na kukimbia nayo msituni.