1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Waziri hewa katika serikali mpya

2 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNQ

Wakati mawaziri katika serikali ya kwanza ya kidemokrasia katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika kipindi cha miongo minne wakichukuwa nafasi zao nafasi moja imeendelea kuwa wazi baada waziri mhusika kushindwa kujitokeza kushika wadhifa wake huo.

Waziri huyo wa biashara Andre Kasongo Ilunga amekuwa akivuma nchini Congo sio kutokana na rushwa au kutumia vibaya madaraka bali iwapo kuwa kweli yuko mtu huyo.

Kutokana na kushindwa kujitokeza kushika wadhifa wake hapo mwezi uliopita Wailunga wengine watatu wamejitokeza kudai wadhifa huo.

Ni watu wachache nchini Congo wanaamini kwamba kweli Ilunga amewahi kuwepo nchini humo na magazeti yamempachika jina kuwa waziri hewa.