1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Benki ya ADB kufadhili miradi ya migodi

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKU

Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB imeikopesha Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo dola milioni laki moja kufadhili mradi wa migodi.Mradi huo wa Tenke Fungurume unahusisha uchimbaji wa madini ya tenke na usafishaji wake ili kupata shaba nyekundu na Kobalti.

Wakati huohuo ukuaji wa uchumi katika taifa hilo unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 6 mwaka huu tofauti na mwaka jana ulipoongezeka kwa asilimia 5.Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Fedha Duniani IMF lililotaraji ukuaji wa asilimia sita u nusu.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa Taasisi hiyo nchini Kongo Xavier Maret,Kongo inapaswa kuzingatia athari za ukuaji wa kiuchumi utakaotokana na mkopo wa bilioni 5 kutoka nchi ya Uchina.Mkopo huo unapangwa kutumika kuimarisha miundo mbinu na sekta ya migodi.