1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:idadi vifo kufuatia mapigano mjini Kinshasa yafikia 150

26 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFH

Idadi ya vifo kufuatia mapigano ya siku mbili katika mji mkuu wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Kinshasa, imefikia 150.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa mjini Kinshasa wanasema kuwa kuna misururu mirefu ya watu nje ya hospitali na nyumba za maiti, huku maiti zaidi zikizidi kuchukuliwa mitaani.

Mapigano hayo kati ya majeshi ya serikali na walinzi wa kiongozi wa upinzani Jean Pierre Bemba ni mabaya zaidi kutokea toka Rais Joseph Kabila aliposhinda uchaguzi mwezi Decemba mwaka jana.

Wanadiplomasia wana wasi wasi kuwa hali hiyo huenda ikadhoofisha maisha ya demokrasia nchini humo.