1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa.Kabila aongoza kwa asilimia 60 ya matokeo .

10 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCu9

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa leo asubuhi, kufuatia duru ya pili ya uchaguzi wa rais katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rais anaemaliza muda wake Joseph Kabila anaongoza kwa asilimia 60.7, dhidi ya asilimia 39.3 za Jean –Piere Bemba baada ya kuhesabiwa kura kutoka vituo 112 kati ya 169 vya upigaji kura.

Hata kabla ya matokeo jumla kujulikana, kambi ya Jean-Piere Bemba anazungumzia juu ya makosa na udanganyifu.

Kamisheni kuu ya uchaguzi inatazamiwa hii leo kuchunguza madai ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na baadhi ya makosa yaliyotokea.

Leo Adhuhuri, kundi la vijana lilitia moto mipira ya magari mjini Kinshasa.

Polisi waliojaribu kuwatawanya vijana hao walirushiwa mawe.

Matokeo rasmi yanatazamiwa kutolewa hadi ifikapo November 19 ijayo.