1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Kipindupindu chazuka Nord Kivu

2 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ac

Ugonjwa wa Kipindupindu unaripotiwa kuzuka mjini Goma ulio mashariki mwa Kongo jambo linalozua hofu ya ugonjwa huo kusambaa katika kambi za wakimbizi wa ndani katika eneo hilo.Maopigano kati ya waasi na wanajeshi wa serikali yamesababisha zaidi ya watu laki tatu u nusu kuyahama makazi yao katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini.

Zaidi ya watu alfu 45 wameachwa bila makazi na wanishi katika kambi za wakimbizi wa ndani karibu na mji wa Goma ambako mashirika ya misaada yanajitahidi kuimarisha usafi.

Kwa mujibu wa shirika la madaktari la Medicins Sans Frontiere watu 533 wameripotiwa kushikwa maradhi ya kipindupindu katika kambi wanazotoa misaada aidha mjini Goma katika kipindi cha majuma sita yaliyopita.