1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa:Makaburi ya Halaiki yagundulikana huko Kongo.

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpj

Wachunguzi wa umoja wa mataifa wamegundua makaburi walimozikwa halaiki ya watu katika mkoa wa mashariki wa Ituri, Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

Taarifa zilisema makaburi hayo yalikua na jumla ya maiti 30.

Wengi ni wanawake na watoto ambao walipotea mapema mwaka huu na sasa inafikiriwa huenda waliuwawa kati ya Agosti na Oktoba.

Maafisa wawili wa polisi wamekamatwa kuhusiana na kutoweka kwa watu hao.