1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Mgombea aliyeshindwa kwenye uchaguzi Kongo kushtakiwa

21 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChZ

Mgombea aliyeshiriki katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa hivi karibuni nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo Marie Teresa Nlandu Nene anatarajiwa kushtakiwa hapo kesho katika mahakama ya kijeshi kwa tuhuma za uchochezi wa ghasia , kuhusika katika uteketezaji moto jumba la mahakama kuu na kumiliki silaha.

Hayo ni kwamujibu wa wakili wake.

Marie alianguka uchaguzi huo kwenye duru ya kwanza iliyofanyika July 30 na kumuunga mkono mgombea aliyeshindwa kwenye duru ya pili ya Uchaguzi huo wa rais Jean Pierre Bemba.Wakili wa Marie Joseph Mukendi amesema hatua hiyo inachukuliwa kisiasa na kwamba mteja wake hana hatia.

Marie alikamatwa Novemba 21 mjini Kinshasa.

Wakati huo huo jeshi la Kongo na kiongozi wa waasi Laurent Nkunda wamefikia makubaliano ya kuwahakikishia raia uhuru wa kutembea kwenye eneo la Mashariki mwa Kongo.