1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Mtuhumiwa wa uhalifu wa kivita apelekwa The Hague

18 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Em

Kiongozi wa kundi la wanamgambo katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo amehamishiwa katika mahakama ya kimataifa ya mjini The Hague nchini Uholanzi.

Germain Katanga alieliongoza kundi la wanamgambo la FRPI amesafirishwa leo kutoka mjini Kinshasa kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa mahakama ya kimataifa.

Kundi la wapiganaji la FRPI lilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2002 kutoka kwenye makabila ya Landu na Ngiti na linatuhumiwa kuhusika na mauaji ya halaiki dhidi ya kabila la Hema.

Katanga anakabiliwa na mashtaka matatu yanayohusiana na uhalifu wa kivita na ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Mtuhumiwa huyo Germain Katanga alikamatwa tangu mwaka 2005 katika mji mkuu wa Kinshasa.