1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Mwanadiplomasia wa Rwanda amewasili Kongo

3 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTB

Mwanadiplomasia kutoka Rwanda amewasili nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika juhudi za kutafuta mbinu za kuwadhibiti waasi wa Rwanda wanao endeleza mapigano katika jimbo la mashariki ya Kongo.

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Charles Murigande anatarajiwa kukutana na rais Joseph Kabila katika ziara yake hiyo ya siku tatu nchini Kongo.

Wasimaizi wa umoja wa mataifa wanasema ziara ya mwanadiplomasia huyo huenda ikasaidia kuleta utulivu.

Hali ya wasiwasi imekumba eneo la Kivu ya kaskazini katika wiki za hivi karibuni kutokana na mvutano kati ya majeshi ya serikali na waasi wanaomuunga mkono jemadari muasi Laurent Nkunda.

Jenerali Nkunda amesema anawalinda watu wake wachache wa kabila la Tutsi katika maeneo ya Kivu ya Kaskazini na Kusini dhidi ya waasi wa Rwanda wa kabila la Hutu wa kundi la FDLR ambalo analaumu kuwa linaungwa mkono na serikali ya Kongo.