1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Watoto waachiwa na Mayi Mayi

18 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIm8

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF limesema watoto zaidi ya mia mbili wameachiwa nchini Jamhuri wa kidemokrasi ya Kongo.

Watoto hao walikuwa wanashikiliwa na waasi wa Mayi Mayi kaskazini mwa jimbo la Kivu.Lakini shirika hilo limeeleza kuwa waasi hao bado wanawashakilia watoto wengine.

Asasi hiyo iliweza kuwakomboa watoto hao kutokana na msaada wa shirika jingine la watoto pamoja na majeshi ya Umoja wa Mataifa yanayolinda amani nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo-Monuc.

Kutokana na mgogoro wa kaskazini mwa jimbo la Kivu kuzidi kupambana moto, watoto wanaorodheshwa kuwa wapiganaji na makundi kama ya Mayi Mayi.