1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyang'anyiro cha Champions League kazi imeanza

30 Agosti 2013

Makundi ya Champions League yapangwa, kazi imebakia kwa makocha kupanga mbinu za kujinusuru katika awamu hiyo, mkurugenzi wa spoti wa mabingwa Bayern Munich Matthias Sammer asema inawezekana kutetea ubingwa wao.

https://p.dw.com/p/19ZHE
ARCHIV - Der Europa-League-Pokal steht am 10.08.2012 auf einem Podest bei der Auslosung für die Europa League in Nyon. Für sieben Bundesliga-Teams wird es am 20.12.2012 spannend: Sie bekommen bei der Auslosung in Nyon ihre Gegner für die nächste Runde in der Champions und Europa League. EPA/MAXIME SCHMID +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kombe la UlayaPicha: picture-alliance/dpa

Awamu ya makundi ya UEFA Champions League inaikutanisha miamba miwili ya soka barani Ulaya pamoja na mapambano mengine ya kusisimua baada ya makundi hayo kupangwa siku ya Alhamis. pamoja na hayo kumekuwa na hali ya utabiri juu ya timu gani inaweza hatimaye kufuzu kupita katika awamu hiyo.

Mpambano kati ya Real Madrid na Juventus Turin katika kundi B na AC Milan na Barcelona katika kundi H huenda ukawa wa kuvutia sana hasa ukiangalia historia ya vilabu hivyo , lakini si ya kuvutia hivyo ukiangalia kwa jumla kuhusu mtazamo wa makundi yao.

epa03842187 UEFA competition director Giorgio Marchetti conducts the draw ceremony for the UEFA Champions League group stage at Grimaldi Forum in Monaco, 29 August 2013. EPA/SEBASTIEN NOGIER
Upangaji wa makundi ya Champions League MonacoPicha: picture-alliance/dpa

Sherehe hiyo ya upangaji wa awamu ya makundi siku ya Alhamis , imeleta msisimko zaidi kuliko hali halisi ya michezo yenyewe ambapo timu kutoka ligi ndogo za mataifa ya ulaya zimefunikwa na vigogo vya soka katika bara la Ulaya .

Hakuna timu rahisi

Pamoja na maneno kama "hakuna timu rahisi" na "timu zote ziko sawa katika kundi fulani" , hayaondoi ukweli kwamba Manchester United , Real Madrid , Chelsea, Juventus , AC Milan , Barcelona , Bayern Munich , Borussia Dortmund ama Paris St. Germain zitashindwa kuingia katika duru ya timu 16 bora.

Awamu ya makundi msimu uliopita ulikuwa na matukio machache ya mshangao na nafasi 13 kati ya 16 katika awamu ya mtoano zilikuwa zimekwisha amuliwa wakati bado duru moja ya mchezo.

lakini pamoja na hayo njia ya timu kama Bayern Munich kuelekea katika utetezi wa taji hilo katika awamu hii ya makundi sio rahisi hivyo.

Kwa Bayern Munich inawasubiri katika kundi D, Manchester City na ZSKA Moscow pamoja na Viktoria Pilsen ambayo inaonekana karatasini kuwa si kikwazo hivyo , miongoni mwa vigingi kuelekea lengo la fainali hapo tarehe 24 Mei 2014 mjini Lisbon. Mkurugenzi wa spoti wa Bayern Munich Matthias Sammer anasema kuwa timu yake ina uwezo wa kutetea taji hilo.

"Samahani, sisi ni mabingwa watetezi. Ni dhahiri kuwa inawezekana kulitetea taji letu, na hilo ndio lengo letu. Kwa upande mwingine Manchester City ni kigongo, wamejiimarisha vya kutosha , na wana kocha mpya. hizi timu nyingine mbili pia sio za kubeza".

Sport director of FC Bayern Munich Matthias Sammer is seen during the UEFA Champions League semi final second leg soccer match between FC Barcelona and FC Bayern Munich at Camp Nou Stadium in Barcelona, Spain, 01 May 2013. Photo: Andreas Gebert/dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mkurugenzi wa spoti Bayern Munich Matthias SammerPicha: picture-alliance/dpa

Utaratibu ni kwamba , hata kama kunatokea mshtuko, vigogo bado vinanafasi ya kusonga mbele kwasababu kuna michezo mingine mitano ambayo wanaweza kujiweka vizuri.

Europa League

Upangaji wa makundi katika kinyang'anyiro cha ligi ya Ulaya , Europa League umefanyika jana na timu mbili za Ujerumani zilizosalia katika ligi hiyo, Eintracht Frankfurt na Freiburg zimepangwa katika makundi ya H na F. Freiburg itapambana na Sevilla, Estoril na Slovan Liberec , wakati Eintracht Frankfurt kundi lake la F lina timu za Bordeaux ya Ufaransa, Maccabi Tel Aviv na APOEL Nicosia.

Kundi A lina timu za Valencia , Swansea City , Kuban Krasnodar na St. Gallen. Tottenham Hotspurs imo katika kundi moja na Anzhi Makhachkala , Sheriff na Tromso. Wigan Athletic , imo katika kundi moja na Rubin Karzan, Maribor na Zulte Waregem.

Bildnummer: 14175278 Datum: 09.08.2013 Copyright: imago/EQ Images Nyon, 09.08.2013, Fussball, Auslosung Champions League Playoffs, Das Los des FC Metalist Kharkiv (UKR) wird gezogen PUBLICATIONxNOTxINxSUIxAUTxLIExITAxFRAxNED ; Fussball Champions League EC 1 2013 2014 Quali Playoff Play Off Auslosung xns x0x 2013 quer premiumd Auslosung Champions League draw Football Fussball Los tirage au sort UEFA barrage Play-off Image number 14175278 date 09 08 2013 Copyright imago EQ Images Nyon 09 08 2013 Football Lots Champions League Playoffs the Los the FC Metalist Kharkiv UKR will considered Football Champions League EC 1 2013 2014 Qualif Playoff Play Off Lots xns x0x 2013 horizontal premiumd Lots Champions League Draw Football Football Los Tirage Au Location UEFA Barrage Play Off
Upangaji wa makundi ya Europa LeaguePicha: Imago

CAF Champions League

Kwa upande wa bara la Afrika katika champions League, Club Zamalek ya Misri italazimika kusaka ushindi kufa na kupona dhidi ya wageni wao kutoka Afrika kusini Orlando Pirates mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa nne wa CAF Champions League.

Licha ya kuwa mataji manne yanawaweka mashujaa hao weupe , Zamalek katika nafasi ya pili ya mafanikio katika kinyang'anyiro hicho nyuma ya majirani zao na mahasimu wakubwa National Al-Ahly, lakini hawajashinda mchezo wowote wa makundi katika miaka mitano iliyopita.

epa03817806 The match fixtures are shown on an electronic panel following draw of the play-offs games of UEFA Champions League 2013/14 at the UEFA Headquarters in Nyon, Switzerland, Friday, August 9, 2013. EPA/LAURENT GILLIERON +++(c) dpa - Bildfunk+++
Timu zilivyopangwa katika makundi ya Champions LeaguePicha: picture-alliance/dpa

Zamalek ilisherehekea ushindi wake wa mwisho dhidi ya Dynamo kutoka Zimbabwe, na kwenda michezo 12 bila ya ushindi tangu wakati huo wakati mahasimu wao Al-ahly waliiteka Afrika mara mbili na kufikia idadi ya mataji saba.

Mashujaa hao wako mwishoni mwa msimamo wa kundi lao la A wakiwa na point moja kutokana na sare waliyoipata katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya mahasimu wao Al-Ahly kabla ya kukubali kipigo dhidi ya AC Leopards ya Congo Brazaville na kuchambuliwa kama karanga na Pirates ya Afrika kusini kwa kuchabangwa mabao 4-1.

kipigo hicho mjini Soweto kina maana kuwa Zamalek inahitaji kujipatia point za kutosha ili kuweka matumaini yao hai katika mji wa kitalii wa bahari ya Sham wa El-Gouma kesho Jumapili.

Mchezaji bora Ulaya

Mchezaji wa kiungo wa mabingwa watetezi wa UEFA Champions League Bayern Munich , Frank Ribery ameteuliwa siku ya Alhamis wiki hii kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Ulaya kwa mwaka 2012/13. Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa ni wa tatu kushinda tuzo hiyo , washindi wengine wa hapo zamani wakiwa ni Lionel Messi wa Barcelona mwaka 2011 na Andres Iniesta mwaka 2012. Ribery ameshinda tuzo hiyo akimshinda Messi na mshambuliaji wa Ureno na Real Madrid Cristiano Ronaldo.

Schalke 04 imemfungisha mkataba wa miaka minne mchezaji wa kati mzaliwa wa Ujerumani na raia wa Ghana Kevin Prince Boateng jana Ijumaa kutoka AC Milan. "Ninafuraha kurejea nyumbani" , amesema Boateng , ambaye baba yake ni Mghana na mama yake Mjerumani.

Boateng mwenye umri wa miaka 26, ambaye pia aliwahi kuichezea Hertha BSC Berlin ya Ujerumani , Portsmouth, na Tottenham Hotspurs zote za Uingereza , na Borussia Dortmund , na ambaye pia ni ndugu yake Jerome Boateng wa Bayern Munich alijiunga na AC Milan mwaka 2010.

Mshambuliaji wa Cameroon Samuel Eto'o amejiunga na Chelsea kwa mkataba wa mwaka mmoja, klabu hiyo ya Premier league imesema jana.

Guardiola

Naye kocha wa mabingwa wa Ulaya Pep Guardiola amesema kuwa angependa kufanyakazi nchini Uingereza wakati fulani. Ameyasema hayo kabla ya mpambano wa UEFA Super Cup dhidi ya Chelsea ya Uingereza.

Mhispania huyo alichukua nafasi ya Jupp Heynckes aliyeitawaza Bayern Munich mabingwa wa EUFA Champions League na kusema angependa kufanyakazi nchini Uingereza katika wakati wake kama kocha. najihisi kuwa ni kocha mchanga , nikiwa na umri wa miaka 42, lakini baadaye nataka kwenda Uingereza, Guardiola amewaambia waandishi habari siku ya alhamis.

Uhamisho wa wachezaji ni uporaji

Wakati huo huo rais wa shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA Michel Platini ametoa wito wa kufanyia mageuzi uhamisho wa wachezaji , akiuita mfumo wa sasa kuwa ni "uporaji".

UEFA president Michel Platini announces the host of the Euro 2016 soccer tournament in Geneva, Switzerland, Friday, May 28, 2010. France will host the 2016 European Championship. (AP Photo/Michael Sohn)
Michel PlatiniPicha: AP

Wakati Real Madrid iko ukingoni mwa kulipa euro milioni 100 kwa ajili ya mchezaji Gareth Bale , Platini amesema tunahitaji kufanya mabadiliko. Nafikiri uhamisho wa wachezaji ni uporaji, amesema Platini. Nafikiri ni nafasi kwa genge la watu kupata fedha nyingi. Leo hii mchezaji ni bidhaa badala ya mchezaji mpira ambapo genge la watu wanajaribu kupata kamisheni.

FIFA na UEFA zinapaswa kuchukua hatua na kupata kitu bora zaidi, amesema rais huyo wa UEFA, Platini. Pia Platini amerejea uungaji wake mkono wa kuhamisha michezo ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 nchini Qatar kuwa wakati wa majira ya baridi ili kuepuka joto kali katika taifa hilo la ghuba.

Nao mji wa Munich umeteuliwa kugombea kuwa mwenyeji wa michezo ya soka ya mataifa ya Ulaya ya Euro 2020 na kuushinda mji wa Berlin. bodi ya shirikisho la kandanda nchini Ujerumani DFB iliuteua uwanja wa mjini Munich wa Allianz Arena wenye uwezo wa kukaa mashabiki 69,000 dhidi ya uwanja wa Olimpiki wa berlin wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 74,000. Mashindano hayo katika mwaka 2020 yatafanyika katika nchi 13.

Wakati huo huo Bastian Schweinsteiger amechaguliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani licha ya maumivu katika kifundo cha mguu , na wachezaji wenzake wa Bayern Munich Toni Kroos na Mario Goetze pia wamerejea kundini katika kikosi hicho kwa ajili ya michezo miwili ya kufuzu katika fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil. kocha Joachim Loew ameteua kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mchezo wa hapo Septemba 6 mjini Munich dhidi ya Austria na Septemba 10 dhidi ya visiwa vya Faroe.

Mchezaji huyo muhimu katika kikosi cha kocha Joachim Loew, amecheza michezo mitatu tu ya timu ya taifa kutokana na kusumbuliwa na maumivu tangu mwaka 2012 baada ya kombe la Ulaya.

Riadha.

Usain Bolt alilazimika kufanya kazi ya ziada kushinda mbio za mita 100 kwa sekunde 9.90 katika michezo ya ligi ya Diamond siku ya Alhamisi. Bolt ilibidi kuuma meno na kukaza misuli ambapo aliweza kumpiku Mjamaica mwenzake ilipofika mita 85 na kumshinda Nickel Ashmeade , ambaye alikuwa wa pili kwa kutumia sekunde 9.94.

Usain Bolt of Jamaica celebrates after winning the men's 200m final at the 14th IAAF World Championships in Athletics at Luzhniki Stadium in Moscow, Russia, 17 August 2013. Photo: Michael Kappeler/dpa
Usain BoltPicha: picture-alliance/dpa

Nae Meseret Defar alichomoka kama mshale katika duru ya mwisho ya mbio za mita 5,000 na kumshinda Turunesh Dibaba katika Diamond league siku ya Alhamisi. Defar bingwa wa dunia na mshindi mara mbili wa michezo ya olimpiki , alimaliza kwa dakika 14, sekunde 32.83, wakati Dibaba mwenye umri wa miaka 28 bingwa mara tatu wa olimpiki na ambaye alifanikiwa kushinda mbio hizo za mita 5,000 na 10,000 mjini Beijing miaka mitano iliyopita akishika nafasi ya pili.

Kwa taarifa hiyo mpenzi msikilizaji ndio sina budi kusema tumefikia mwisho wa kuwaletea habari hizi za michezo, hadi mara nyingine - Kwaherini.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / ape / rtre / dpae /

Mhariri: Mohammed Khelef