1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyang'anyiro cha kombe la mataifa ya Afrika kuanza leo

Sekione Kitojo20 Januari 2012

Kinyang'anyiro cha kuwania ubingwa wa mataifa ya Afrika kinaanza rasmi leo jioni. Guinea ya Ikweta na Gabon ziko tayari kwa tamasha hilo la 28 la michezo katika bara la Afrika.

https://p.dw.com/p/13nLc
Orange Africa Cup of Nations. Die 28. Fußball-Afrikameisterschaft 2012 (Africa Cup oder engl.: Africa Cup of Nations), organisiert vom afrikanischen Verband Confédération Africaine de Football (CAF), findet in Gabun und Äquatorialguinea statt.[1] Wie bei der vergangenen Afrikameisterschaft treten zusammen mit den Gastgebern 16 Mannschaften zunächst in Gruppen und danach in Ausscheidungsspielen gegeneinander an. Insgesamt werden 32 Spiele ausgetragen.
Nembo ya mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2012

Kwa wapenzi wa mchezo maridadi wa soka macho pamoja na masikio yanaelekezwa katika wiki tatu zijazo huko Gabon na Guinea ya Ikweta ambako kuanzia leo jioni nchi hizo jirani zenye utajiri mkubwa wa mafuta zinakuwa wenyeji wenza wa mashindano ya 28 ya kombe la mataifa ya Afrika.

Kama chakula maalum cha heshima kilichoandaliwa na kiongozi wa nchi bila ya kuwa na mgeni mashuhuri, tamasha hili la soka linafanyika bila ya kuwapo vigogo vya soka kama Mafarao wa Misri, ambao ni mabingwa wa mashindano hayo katika fainali tatu zilizopita.

Vigogo wengine wa soka kama Cameroon , Nigeria na Afrika kusini pia hawamo katika kinyang'anyiro hiki mwaka huu.

Kutokana na kutokuwapo kwa vigogo hivi vinne vya soka katika tamasha la mwaka huu, Ghana ambayo imefikia robo fainali ya kombe la dunia pamoja na Didier Drogba akiwa na Cote D'Ivoire ni timu zinazoonekana kuweza kutoroka na kombe hilo ambalo limewakimbia kwa muda mrefu sana.

Ghana's Andre Ayew looks on in a line-up before the start of their pre-World Cup soccer match against Latvia at Stadium MK in Milton Keynes, England, Saturday June 5, 2010. Ghana is preparing for their South Africa World Cup which begin on June 11. (AP Photo/Sang Tan)
Mchezaji Andre Ayew wa GhanaPicha: AP

Guinea ya Ikweta itafungua pazia la michuano hii jioni ya leo dhidi ya Libya mjini Bata ikiwa na nia zaidi ya kulinda hadhi ya taifa. Mtoto wa rais wa nchi hiyo Teodoro Obiang amewaahidi wachezaji wa Guinea ya Ikweta kitita cha dola milioni moja kila mmoja ili kuweza kushinda pambano hilo la ufunguzi la mataifa ya Afrika na kiasi cha dola 20,000 kwa kila goli litakalotumbukizwa wavuni.

Heshima na sio fedha , ndio kitu kinachoisukuma Ghana na Cote D'Ivoire kusaka ushindi mara hii.

Ghana ililinyakua kombe hilo mara ya mwisho miaka 30 iliyopita wakati ilipoilaza Libya kwa mikwaju ya penalti. Kocha Goran Stevanovic amesema kuwa , timu yake ilikuwa makamu bingwa wa kombe hilo nchini Angola miaka miwili iliyopita na kufikia katika kiwango hicho tena sio jambo linalokusudiwa.

Katika bundesliga leo unaanza mchezo wa wiki ya 18, ambapo Nuremberg inakwaana na Hertha BSC Berlin, Hoffenheim , inaikaribisha Hannover 96, Freiburg itakuwa kibaruani dhidi ya Augsburg na Schalke ina miadi na VFB Stuttgart. VFL Wolfsburg inakutana na FC Koln ,wakati Kaiserslautern itakuwa kazini dhidi ya Werder Bremen. Kesho Jumapili mabingwa watetezi Borussia Dortmund inakwenda nyumbani kwa Hamburg wakati Bayer Leverkusen ina miadi na Mainz 05.

Na katika ligi ya Uingereza Premier League jioni ya leo Bolton Wanderous ina kwaana na Liverpool, Everton inatiana kifuani na Blackburn Rovers, Fulham ina miadi na Newcastle United, na Norwich inaikaribisha Chelsea. Wigan na Queen park rangers wataonyeshana nani zaidi , Stoke City wanaivaa West Brom, na Sundeland itakuwa kibaruani na Swansea City, wakati Aston Villa ikiwa mgeni wa Wolves.

Jumapili ni Manchester United na Arsenal wakati Manchester City ikiikaribisha timu nyingine kutoka mjini London Tottenham Hot Spurs.

epa02586616 Arsenal's Robin van Persie (L) celebrates with his team mates after scoring the 1-1 equalizer against FC Barcelona during the UEFA Champions League round of 16 match at Emirates Stadium in London, Britain, 16 February 2011. EPA/ANDY RAIN +++(c) dpa - Bildfunk+++
Wachezaji wa Arsenal London ambao wanakutana na Mnchester United kesho JumapiliPicha: picture-alliance/dpa

Na katika riadha , Ethiopia imewapiga marufuku wanariadha 35 , ikiwa ni pamoja na Kenenisa Bekel kushiriki mashindano yoyote kutokana na mzozo kuhusu mazowezi, amesema afisa wa riadha nchini humo jana.

Nae mwanariadha wa Uingereza Bernice Wilson amepigwa marufuku kushiriki riadha kwa miaka minne baada ya kushindwa rufaa yake dhidi ya adhabu , ambayo alipewa baada ya kugundulika kuwa anatumia madawa ya kuongeza nguvu.

Wilson mwenye umri wa miaka 27 , aliingia katika kiwango cha kimataifa katika mashindano ya riadha ya Ulaya mjini Paris March mwaka jana lakini kupanda kwake kwa haraka kuliishia ukingoni wakati alipogundulika kutumia madawa hayo Juni 12 mwaka jana.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae

Mhariri : Yusuf Saumu