1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyang'anyiro cha soka cha EURO 2008 chaanza

Kalyango Siraj10 Juni 2008

Ujerumani yapata ushindi wa kwanza

https://p.dw.com/p/EGDx
Lukas Podoski,alifunga mabao mawili ya timu ya UjerumaniPicha: AP

Mashindano ya soka kuwania ubingwa wa Ulaya mwaka huu wa 2008 yalianza rasmi mwishoni mwa juma nchini Austria ambapo mechi nne zilichezwa.

Katika matokeo ya mojawapo wa mechi za mwishoni mwa juma,timu ya soka ya Ujerumani iliweza kuilaza Poland mabao mawili bila jibu katika fungua dimba la kundi B.

Mabao yote mawili yalipachikwa wavuni na mshambuliaji,Lukas Podolski kunako dakika za 20 na 72. Baada ya mechi nahodha wa Ujerumani Michel Ballack alisema kilichowafanya kupata ushindi huo licha ya timu waliokuwa wakicheza nayo ilikuwa si kidogo.'tumecheza kwa ustadi na tulifanya makosa machache.Tulifanikiwa kupata bao la kwanza na hilo ndilo lilikuwa muhimu.’

Nae mfungaji wa mabao hayo, Podoski ,alisema kuwa walicheza vizuri kutokana na mipango yao ilivyokuwa. Hata hivyo hakufurahi sana wakati alipofunga bao. Je alihisi kuwa alikuwa ameotea? Anatoa jibu.

'Ninafamilia kubwa nchini Poland.Nimezaliwa huko na ninaiheshimu nchi hiyo.na hiyo ndio sababu ilionifanya niwe katika hali hiyo baada ya kufunga bao.’

Ushindi huu wa Ujerumani ndio wa kwanza katika mashindano hayo wakati walipoishinda Jamhuri ya Czech kuweza kutwa ubingwa wa mwaka 1996 katika uwanja wa Wembley.Na pia unaifanya timu hiyo kuongoza kundi hilo ikiwa na pointi tatu na mabao mawili. Inafuatiwa na Croatia ambayo nayo, katika mechi yake ya ufunguzi hapo jana, iliishinda mwenyeji Austria bao moja kwa bila .

Ushindi wa Croatia wa mwishoni mwa juma ndio wa kwanza kwa kipindi cha miaka sita katika mashindano makubwa kama hayo.Mara ya mwisho kushinda ilikuwa wakati wa mashindano ya kombe la dunia ya mwaka wa 2002 waliposhinda Italy mabao mawili kwa moja.Pia ilikuwa haijawahi kushinda mechi yake ya kwanza ya mashindano kama hayo tangu mashindano ya kombe la dunia yaliyofanyika Ufaransa katika kombe la mwaka wa 1998.Wakati huo waliwalaza wenzao kutoka jamaica tatu kwa moja, katika mashindano ambapo walishika nafasi ya tatu.

Hii ndio mara ya 33 Ujerumani ikishirika katika mashindano hayo huku Poland hii ndio mara yake ya kwanza.Ujerumani inacheza tena alhamisi dhdi ya Croatia.

Katika kundi A Jamhuri ya Czech nayo ilipata ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Uswisi.Pia katika kundi hilo Ureno iliigaragaza Uturuki mabao 2 kwa nunge.na katika kundi hilo Ureno ndio inaongoza ikiwa na pointi tatu na mabao mawili.Jamhuri ya Czech ni ya pili na pointi tatu na bao moja.

Mashindano ya mwaka huu ambayo yameandaliwa na nchi mbili Ushiwisi na Austria

Leo Jumatatu ni zamu ya Uswisi kuchezesha mechi zake za kundi C lenye timu kama vile Ufaransa,ambayo leo inaingia uwanjani dhidi ya Romania katika mji wa Zurich. Pia Uholanzi inakutana dhidi ya mabingwa wa kombe la dunia wa Italy.

Kwa mda huohuo jana jumapili wanausalama wa Austria, waliwatia mbaroni mashabiki 140 na ushei, wengi wao wakiwa raia wa Ujerumani katika mji wa Klagenfurt, baada ya kupambana dhidi ya mashabiki wenzao wa Poland.