1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyan'ganyiro cha tikiti za finali za Kombe la Ulaya na Afrika 2008 uwanjani

Ramadhan Ali6 Oktoba 2006

Timu kadhaa za kitaifa zinaingia uwanjani mwishoni mwa wiki hii kuania tiketi za finali 2-moja ya kombe la Ulaya la Mataifa 2008 huko Uswisi na lile la Afrika nchini Ghana.Katika mbio za magari,Michael Schumacher atazamia kutamba huko Suzuki,Japan na kutoroka na taji la 8 mwishoni mwa msimu huu.

https://p.dw.com/p/CHd5

Kombe la Aftika la mataifa:Timu kadhaa za taifa za Africa ziko uwanjani leo na kesho kuania tiketi zao za finali ya Kombe la Afrika litakaloaniwa nchini Ghana, 2008:

Nafasi ya Afrika Kusini,mwenyeji wa kombe lijalo la dunia kushiriki huko Ghana-miaka 2 kabla kuandaa Kombe la dunia ,zitategemea iwapo Bafana Bafana, watawika kesho mbele ya Zambia.Kwani, wakishindwa, watajikuta pointi 5 nyuma ya viongozi wa kundi hili la 11-wenyeji wao zambia.

Kocha wa zamani wa Brazil,Alberto Parreira ,atakaeanza rasmi kazi yake hapo Januari,mwakani, ameafuatana na Bafana Bafana kwenda Lusaka.

Afrika Kusini ilizimwa 0:0 nyumbani na Kongo katika mpambano wao wa kwanza wakati mahasimu wao kesho Zambia, waliilaza Chad kwa mabao 2:0.Isitoshe, Afrika Kusini inacheza kesho bila ya mshambulizi wake hatari Beni McCarthy, aliekataa mwito wa kjiunga na kikosi uliotolewa na kocha wa kujishikiza Pitso Mosimane.

Kumekuwapo pia shakashaka iwapo stadi mwengine anaeicheza katika Bundesliga-Ligi ya Ujerumani, Sibusiso Zuma ,kwavile klabu yake ya Ujerumani Armenia Bielefeld,haitaki kumuona akicheza.Kwani, baada ya kuumia kwa miezi 6 ,Zuma alirejea uwa njani mwishoni mwa wiki iliopita na apatia bao.

Togo iliowakilisha africa katika Kombe la dunia, ikitumai kuimshawishi stadi wake anaeichezea Arsenal, Emmanuel Adebayor kurudi katika timu ya Taifa baada ya kukataa kucheza mpambano uliopiota dhidi ya Benin kwa manunguniko ya fedha za nwakati wa kombe la dunia.Togo ina miadi na Mali kesho mjini Bamako.

Corte d’Iviore au Ivory Coast chini ya kocha mjerumani,Uli Stielike,inaikaribisha Gabon kesho mjini Abidjan.Stielike amezusha msangao kwa kumuacha mshambulizi hatari Bonaventure Kalou-nahodha wa zamani wa Tembo wa Ivory Coast.Hii ni mechi ya kwanza kwa Corte d’Iviore tangu ilipopigwa kumbo katika duru ya kwanza ya Kombe lililopita la dunia hapa Ujerumani.

Simba wa nyika –Kamerun watakuwa bila ya mshambulizi wao Samuel Eto’o watakapokutana nyumbani na Guinea ya Ekweta.Mlinzi wa Werder Bremen,Pierre Wome amekataa nae nafasi ya kujiunga na simba wa nyika kwa changamoto ya kesho-hii ni kwa muujibu wa kocha wa Kamerun, Arie Haan. Kamerun ilitandika Ruanda mabao 3:0 nyumbani katika duru yao ya kwanza .Nigeria wamefunga safari ya Lesotho.

Kwa mashabiki wa dimba wa Afrika mashariki macho yanakodolewa changamoto kati ya Tanzania na Msumbiji,mjini Maputo na Kenya na Angola mjini ,Luanda:

Bafana Bafana iliteleza nyumbani ilipotoka 0:0 na Kongo-Brazzaville.Lazima itambe Lusaka mbele ya Zambia.

Ulaya pia kinyan’ganyiro cha kuania tiketi za finali ya 2008 nchini Uswisi kinaendelea:

Ujerumani chini ya kocha mpya Joachim Loew, inacheza nyumbani Rostock na Georgia.Majirani zao Holland wanaonana na Bulgaria bila ya mshambulizi stadi Van Niestelrooy wa Real Madrid na Mark van Bommel wa Bayern Munich aliejiunga na Niestelrooy kumpinga kocha Marco van Basten.

Makamo-bingwa wa dunia-Ufaransa wamemuita tena Nicolas Anelka kujiunga na kikosi kinachopambana na Scotland.Ufaransa inabidi kucheza na kipa mwengine, kwavile, kipa wao maarufu Fabien Barthez ameamua kustaafu.

Mabingwa wa dunia Itali ,wanakutana na Ucraine lakini watabidi kuchunga kufuatia kuteleza duru ya kwanza.

MBIO ZA MAGARI: keshokutwa jumapili asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mkutano Suzuki,Japan:huko Michael Schumacher wa Ujerumani anatapia taji lake la 8 la ubingwa wa dunia na baada yxa kumpiku hasimu yake Alonso –mspain huko Shanghai,China, mwishoni mwa wiki iliopita,Schumacher anajua akitamba tena kesho taji la 8 ni lake.

Tatizo kubwa wakati huu katika michezo hasa ya malino-professional sports ni madhambi ya doping-matumnizi ya madama kutunisha misuri na kuongeza kasi:

Hivi sasa maabara yanayopigana na vita na madhambi ya doping, yanafanya majaribio ya kugundua unga unaotumiwa na wanariadha kufuta ishara za matuimizi ya dawa ya EPO kwenye mkojo wao wanaotoa wanapokaguliwa.