1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyang´anyiro kati ya Obama na Clinton chapamba moto

3 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1dZ

Seneta Barack Obama na Hillary Clinton wabunge wa chama cha Democratic nchini Marekani wanaowania kugombea urais, wanakaribiana sana katika majimbo ya Carlifonia, New Jersey na Missouri siku mbili kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika katika majimbo 22 nchini humo.

Kwa mujibu wa kura ya maoni Obama anaongoza katika jimbo la Carlifonia na wako sawa na Clinton katika jimbo la New Jersey na Missouri. Obama anaongoza pia katika jimbo la Georgia.

Kwa upande wa chama cha Republican, seneta Mit Romney, ameshinda uchaguzi katika jimbo la Maine katika uchaguzi wa mwisho kabla uchaguzi mkubwa uliopangwa kufanyika Jumanne wiki ijayo.

Gavana huyo wa zamani wa jimbo la Massachuttes ameshinda asilimia 52 ya kura ikilinganishwa na mpinzani wake wa karibu, John McCain, aliyepata asilimia 22.

Ushindi wa Romney katika jimbo la Maine umemuongezea nguvu mwanasiasa huyo baada ya kushindwa na McCaina katika majimbo ya Florida na South Carolina.

Kura ya maoni inaonyesha John McCain anaongoza katika majimbo ya New York, New Jersy na Missouri lakini ameshindwa na Romney katika jimbo la Carlifonia.

Mshindi atakayegombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican atajulikana Jumanne ijayo wakati majimbo 22 yatakapopiga kura, ikiwa ni pamoja na majimbo yenye idadi kubwa ya wakaazi ya California, New York, Illinois na New Jersey.