1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyanganyiro Kombe la dunia

14 Oktoba 2008

Ujerumani ina miadi leo na Wales.

https://p.dw.com/p/FZFl
Kevin KuranyiPicha: AP

Baada ya changamoto za mwishoni mwa wiki kuania tiketi za kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika Kusini,, timu za kanda zote isipokua Afrika, zinarudi uwanjani jioni ya leo. Dola mbili kuu za dimba za Ulaya-mabingwa Spain na Uingereza, zitajaribu leo kuparamia kileleni mwa makundi yao na kupiga hatua nyengine kuelekea Afrika Kusini.

Na huko Afrika Kusini kwenyewe, wajumbe wote wafuasi wa rais wa zamani Thabo Mbeki, wametimuliwa nje ya Kamati ya Maandalio ya Kombe la Dunia.

Mabingwa mara 3 wa dunia-Ujerumani hawatokwi na machozi juu ya kisa cha mshambulizi wao Kevin Kuranyi kuwaachamkono na wamepania kuishinda Wales jioni hii na mwishoe, kukata tiketi yao ya kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika kusini.Wanaingia uwanjani leo bila ya nahodha wao Michael Ballack alieumia ,lakini wakitiwa nguvu na mabao 2-1 dhidi ya urusi hapo jumamosi.

Kuranyi aliomba radhi katika mkutano na waandishi habari akidai alikabiliwa na hali ngumu mnamo miaka 3 iliopita na akiwa kama ni mchezaji anasema yeye pia ni binadamu. Kocha wa Ujerumani Joachim Loew,asema kisa cha Kuranyi kimepita na hatacheza tena katika timu ya Taifa.Kuranyi alifunga virago jumamosi na kuiachamkono timu baada ya kuarifiwa hatacheza katika mpambano na Urusi.

Kocha Loew hana upungufu wa washambulizi:Kuna Lukas podolski alielifumania juzi lango la urusi kwa bao la kwanza.Ana Miroslav Klose,mtiaji mabao mengi kombe lililopita la dunia na ana Mario Gomez wa Stuttgart. Listi gani ataiteremsha uwanjani kocha Loew na iwapo nahodha Ballack atapata nafuu kurudi uwanjani , yafaa kusubiri kuona.Ujerumani inaongoza kundi hili ikiwa na pointi 7 na ushindi leo dhidi ya Wales utawafungulia mwanya wa pointi 4 kileleni.

England au Uingereza wanaoongoza nao kundi la 6 bukheri-mustraehe wakiwa wameshinda mara 3 katika mapambano 3.Jumamosi, waingereza walitamba mbele ya Kazakhastan uwanjani Wembley,walipowachapa wakhazaki mabao 5-1.Ushindi mwengine leo dhidi ya Belorussia utawaimarisha kileleni mwa kundi hilo la 6.

Ama mabingwa wa ulaya-Spain pia hawana shaka kwani hadi sasa hawakuteleza:

Leo wana miadi katika kundi la 5 na wabelgiji. Waspian,mabingwa wa Ulya hawakushindwa katika mechi 26 mfululizo.Mwishoni mwa wiki waliwika huko Estonia kwa ushindi wa mabao 3-0,lakini kocha mpya wa Spian, Vicente del Bosque ameungama mpambano wa leo na Ubelgiji utakua kibarua kigumu.

Katika kanda ya Amerika kusini,viongozi wa kanda hii Paraguay wana miadi na Peru na mabingwa mara kadhaa wa dunia Brazil zamu yao ni kesho kupambana na Colombia.Mahasimu wao Argentina wanacheza na Chile wakati Venezuela iliokomewa mabao 4:0 na Brazil jumapili iliopita, wanaonana na Ecuador.

Wajumbe wote wafuasi wa rais Thabo Mbeki aliejiuzulu huko Afrka Kusini, wamepigwa teke nje ya Kamati ya Maandalio ya Kombe la Dunia 2010.Waziri wa zamani wa serikali za mikoa Mufamadi,makamo wwa zamani wa waziri wa fedha Moleketi na waziri wa zamani afisi ya rais Pahad,wameondoshwa katika kamati hiyo kama waakilishi wa serikali.Hii ni kwa muujibu wa tangazo la serikali ya rais Kgalema Motlanthe.

Rais Motlanthe, amewachagua wajumbe 3 wapya katika kamati hiyo .Hatua hii ambayo haikuwasangaza wengi,inainyima Kamati ya maandalio wajumbe wenye maarifa makubwa tena zikibaki siku 6000 kabla kombe la dunia kuanza Juni,2010.