1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kipangamizi cha mwisho kimeondoshwa na Mahakama Kuu

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQPy

Mahakama Kuu nchini Pakistan imeondosha kipingamizi cha mwisho kumruhusu Rais Pervez Musharraf kuendelea na wadhifa wa rais kwa awamu nyingine ya miaka 5,na hivyo kumfungulia njia ya kujiuzulu kama mkuu wa majeshi.Mahakama hiyo tayari ilikwisha ondosha vipingamizi vingine vitano kuhusika na kuchaguliwa kwake katika mwezi uliopita.Musharraf mara kwa mara amesema, atajiuzulu kama mkuu wa majeshi na ataapishwa kama rais wa kiraia,ikiwa uamuzi wa Mahakama Kuu utamuunga mkono.Rais Musharraf alitangaza hali ya hatari takriban majuma matatu yaliyopita,hatua ambayo imelaaniwa vikali na mataifa mengi.