1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KISMAYU: Mapigano yazuka kusini mwa Somalia

1 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCeN

Mapiganao makali yamezuka nje ya mji wa Jilib kusini mwa Somalia, baina ya wanamgambo wa mahakama za kiislamu na wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia.

Watoa misada ya kiutu wamesema maelfu ya wasomali tayari wamekimbia kutoka mjini humo.

Mji wa bandari wa Kismayu unasemekana ni ngome ya mwisho iliyosalia ya wanamgambo wa mahakama za kiislamu, waliotimuliwa kutoka mjini Mogadishu mnamo Alhamisi iliyopita baada ya kushambuliwa na majeshi ya Ethiopia.