1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kitisho cha wanaostaafu kuishi maisha duni

3 Septemba 2012

Kitisho cha watu kuangukia katika hali ya umaskini wanapostaafu,Kishindo kinachowakabili walinzi wa mazingira katika kuwateuwa watakaewaongoza katika uchaguzi mkuu mwakani ndizo mada kuu magazetini hii leo

https://p.dw.com/p/162Wa
Waziri wa ajira bibi Ursula von der LeyenPicha: dapd

Tuanzie lakini na mada iliyoingia midomoni na kuzusha hofu miongoni mwa raia:Kitisho cha umaskini watu wanapostaafu.Waziri wa ajira Ursula von der Leyen amepania kupambana na kitisho hicho.Anapendekeza kuanzisha ruzuku ya Euro 850 kwa mwezi.Lakini mhariri wa gazeti la "Rhein-Zeitung" anahisi ruzuku hiyo haitasaidia kupambana na chanzuo halisi cha umasikini wa uzeeni.Tatizo hasa anasema linahitaji kufumbuliwa katika soko la ajira.Kiwango cha chini cha fedha tasalimu watu wanazolipwa kinabidi kiongezeke,kwa kuanzishwa kiwango maalum cha mishahara,nafasi zaidi za shule za chekechea,mafunzo bora zaidi ya kazi na kodi haba za mapato.Na zaidi ya hayo mpango wa serikali wa huduma za uzeeni nao pia unabidi ufanyiwe marekebisho ya kina.

Gazeti la "Rhein-Necker-Zeitung" linajiuliza kama kweli mpango wa waziri wa ajira wa kuanzishwa ruzuku maalum katika malipo ya uzeeni,ndio ufumbuzi wa tatizo la watu kuangukia katika hali ya umaskini wanapostaafu.Gazeti linahisi ingawa waziri amechapisha tarakimu za kutisha ili kusaka uungaji mkono wa mpango wake.Ukweli lakini ni kwamba ruzuku hiyo haitasaidia pakubwa katika mfumo jumla wa malipo ya uzeeni uliochakaa ambao hauwasaidii kujikidhia mahitaji yao wale ambao tokea hapo malipo yao ya uzeeni ni haba.

ARCHIV ZU Jürgen Trittin hat seine Kandidatur für die Spitzenkandidatur im nächsten Bundestagswahlkampf erklärt
Jürgen Trittin anapewa nafasi nzuri ya kuchaguliwa kuwaongoza walinzi wa mazingira katika uchaguzi mkuu wa mwakaniPicha: dapd

Mada yetu ya pili magazetini inahusiana na zoezi la walizi wa mazingira kuwachagua wale wanaotaka waongoze orodha yao ya uchaguzi katika uchaguzi mkuu wa mwakani.Gazeti la "Berliner Zeitung linasema hata kama watu watauangalia utaratibu wa walinzi wa mazingira kuwachaguwa viongozi wanne au sita kuwa ni wenye kuchekesha-ukweli lakini ni kwamba chama hicho kinachotanguliza mbele mfumo wa demokrasia unaoanzia tangu katika mashina,kimejipatia umaarufu tangu miaka ya 80 kutokana na utaratibu huo huo .Kimegeuka kuwa chama pekee kati ya vyama mashuhuri vya humu nchini kufuata mfumo huo na kinaweza kwa namna hiyo kutoa mchango wa maana katika medani ya kisiasa nchini Ujerumani.

Gazeti la Straubinger Zeitung linaahisi hata hivyo zoezi la kuwaachia mashina kumchagua mwanasiasa atakaekiongoza chama cha waalinzi wa mazingira Die Grüne katika uchaguzi mkuu wa mwakani linaweza kugeuka machungu kwa mkuu wa tawi la Die Grüne bungeni,bibi Renate Künast.Pindi akishindwa tena,kama alivyoshindwa katika juhudi zake za kutaka kuchaguliwa kuwa diwani wa jiji la Berlin,basi walinzi wa mazingira watakuwa wamemtokomoeza daraja ya pili au hata ya tatu mwanasiasa huyo mashuhuri kupita kiasi.

Mwandishi:Hamidou Oummilkhheir/Inlandspresse

Mhariri Yusuf Saumu